
Uainishaji wa Mafumbo ya Wosia wa Babu kwa Wavulana Miongoni mwa Wabukusu wa Kenya.
Author(s) -
John Swala Barasa Wangila,
Sheila Wandera-Simwa,
Onyango J. Ogola
Publication year - 2021
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Uncategorized
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v3i1.206
Subject(s) - humanities , art
Utafiti huu ulidhamiria kuainishaji mafumbo ya wosia wa babu kwa wavulana miongoni mwa Wabukusu wa Kenya. Madhumuni ya makala hii yalikuwa kuainisha mafumbo yanayotumiwa katika miktadha ya wosia wa babu kwa wavulana miongoni mwa Wabukusu wa Kenya. Uandishi wa makala hii ulitumia nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Leech (1965). Nadharia hii huhimiza umuhimu wa mitindo tofauti ya lugha katika fasihi. Data za Makala zilikusanywa kutoka kata mbili za wilaya ya Kimilili. Muundo wa kimaelezo ulitumika kuwasilisha na kuchanganua data. Mbinu za mahojiano na uchunzaji wa kushiriki zilitumika kukusanya data. Sampuli ya kimaksudi ilitumiwa kuwachagua wazee wanne wa kati ya miaka sitini na sabini na wavulana wanne wa kati ya miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili kutoka kata zizo hizo ili kushiriki katika utafiti. Utafiti ulibainisha kuwa babu hutumia mafumbo ya vitendawili, mafumbo ya jazanda, mafumbo ya majina, mafumbo ya maonyo, mafumbo ya miko na chemshabongo katika wosia wao kwa wavulana. Makala hii ina manufaa kwa wanafunzi na wataalamu wa fasihi simulizi, shuleni na vyuoni, kwa kuwafahamisha kuhusu aina ya mafumbo yanayotumika katika jamii ya Wabukusu na jamii zingine. Makala hii inapendekeza kuwa vyombo vya habari viwe vikupeperusha hotuba za wosia unaotumia mafumbo kwa wananchi ili kuwafikia watu wengi. Kwa kufanya hivi, wavulana wengi watapata ujumbe uliomo kwenye mafumbo haya na wataimarika kitabia.