
Falsafa ya Jazanda ya Uongozi na Mauko katika Methali za Jamii ya Wanyore: Mtazamo wa Kisemantiki
Author(s) -
Henry F. Andele,
Susan Chebet Choge,
Fred S. Wanjala
Publication year - 2020
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Bosnian
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v2i1.175
Subject(s) - physics , humanities , philosophy
Makala hii inatokana na utafiti ambao uliazimia kutathmini falsafa ya jazanda katika methali za Wanyore kwa mtazamo wa kisemantiki. Madhumuni ya makala yenyewe yanahusu falsafa ya uongozi na mauko katika methali za Wanyore. Nadharia ya Uhusiano ya Sperber na Wilson (1986) na iliyoendelezwa nao (2004) ndiyo iliyoongoza makala hii. Nadharia hii ilitumiwa kufafanulia maana za methali katika jamii ya Wanyore. Data ilikusanywa kutoka kwa Wanyore wanaoishi katika kaunti ndogo ya Emuhaya na Luanda katika kaunti ya Vihiga. Makala haya yalitumia njia za uchanganuzi matini na mahojiano kukusanya data. Vifaa vilivyotumiwa vilikuwa ratiba ya usaili na tepurekoda. Data ilichanganuliwa kimaelezo kwa kunukuu methali za Kinyore, kisha zikatafsiriwa na kufasiriwa katika Kiswahili hatimaye falsafa ya jazanda ya uongozi na mauko ikaainishwa na kuelezwa. Matokeo ya kazi hii yatachangia kueleweka kwa falsafa ya jazanda ya uongozi na mauko miongoni mwa wanajamii. Pia, yatakuwa nyongeza ya marejeleo kwa watafiti katika uwanja wa methali.