
Jinsi Vipengele vya Kitamaduni katika Matini Teule ya Kiswahili na Kikalenjin Vilivyochangia Mtafsiri Kuiandika Upya Bukuit Ne Tilil.
Author(s) -
Jane Jepkoech Singoei; Mwanakombo Mohamed; Mosol Kandagor
Publication year - 2020
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v2i1.155
Subject(s) - physics , theology , humanities , art , philosophy
Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya Kiswahili na Kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu, ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubaini kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri. Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa: utamaduni wa Waswahili na wa Wakalenjin ni tofauti na hii ilipelekea uandishi upya ufanywe katika tafsiri. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Sera za elimu kuhusu lugha za kienyeji zinafaa kutilia maanani tafsiri ya matini za kufundishia.