
Usawiri wa Ukombozi katika Diwani ya Euphrase Kezilahabi ya Kichomi: Mtazamo wa Kidhanaishi
Author(s) -
Chibayi Jason Poyi,
Dkt. Sheila Pamela Wandera-Simwa
Publication year - 2020
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Spanish
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v2i1.146
Subject(s) - physics
Makala hii inakusudia kuonyesha namna ukombozi ulivyosawiriwa kama sehemu ya falsafa ya Euphrase Kezilahabi katika diwani yake ya Kichomi. Euphrase Kezilahabi ni mwandishi nguli wa mashairi aliyeasi magwanda ya umapokeo. Mojawapo wa sifa bainishi ya falsafa ya Kezilahabi ni ukombozi, ambayo huifanya kuwa falsafa ya uhuru yenye tafsiri nyingi ambazo ndizo msingi wa makala hii. Tahakiki nyingi kuhusu diwani hii imeshughulikia falsafa ya maisha ya Kezilahabi pasipo kuangazia usawiri wa ukombozi kama sifa bainishi ya mhimili wa uhuru. Makala hii itafafanua usawiri wa ukombozi huu kwa kutumia nadharia ya Udhanaishi iliyoasisiwa na Jean Paul Satre (1970). Sampuli ya makala hii iliteuliwa kimaksudi. Data ya kimsingi itakusanywa kwa njia ya kusoma mashairi katika diwani teule na makala mengine yanayohusiana nayo. Makala hii itachukua muundo wa kimaelezo na data itakayokusanywa itafafanuliwa kwa njia ya maelezo kwa kuegemeza kwenye mhimili wa uhuru wa nadharia ya Udhanaishi. Uchanganuzi wa data wa makala hii utaongozwa na mbinu ya uhakiki matini. Kwa kuwa diwani za mashairi ya Kezilahabi zimekuwa taaluma ya mijadala mipana, makala hii itakuwa mchango mkubwa kwa mijadala hiyo. Itawasaidia wanataaluma ya ushairi kuelewa namna Kezilahabi anavyousawiri ukombozi wa binadamu kwenye mashairi ya diwani ya Kichomi.