z-logo
open-access-imgOpen Access
Upambanuzi wa changamoto za vijana kama inavyodhihirika katika riwaya teule za Walibora
Author(s) -
Harrison Onyango Ogutu; Prof. James Onyango Ogola; Prof. Wendo Nabea
Publication year - 2020
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Bosnian
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v2i1.142
Subject(s) - humanities , philosophy
Utafiti huu ulilenga kubaini changamoto zilizowakabili vijana katika mazingira walimoishi kwa mujibu wa riwaya za Walibora ambazo ni Kufa Kuzikana, Ndoto ya Almasi na Kidagaa Kimemwozea. Utafiti huu ulielekezwa na nadharia ya uhalisia ambayo hushughulikia uwasilishi wa uhalisi na ukweli wa mambo katika fasihi. Imani ya mhalisia ni kwamba kazi ya fasihi huwaweka wanajamii katika ulimwengu wao wa kawaida, kweli na halisi. Mihimili ya uhalisia iliotumika katika utafiti huu ilikuwa; nguzo ya kielelezo inayosisitiza uigaji wa hali halisi kwa njia ya kweli, wazi na sahihi; nguzo ya matumizi ya lugha ya wakati uliopo na inayosheheni uhalisi na ukweli wa mambo kama yalivyo katika jamii husika ilitumika. Njia kuu ya utafiti huu ilikuwa utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo katika ukusanyaji data huku mbinu ya kithamano ikitumika kuchanganua na kueleza data ya visa na matukio yaliyodhihirisha changamoto dhidi ya vijana. Utafiti huu   ulijikita   katika   muundo   wa   kimaelezi   ambao   ni   sahili   na   kueleza   mambo yanavyojitokeza kwa uyakinifu.Utafiti huu ulilenga wahusika vijana katika riwaya za Walibora huku akiangazia changamoto zilizowakabili. Mtafiti alitumia sampuli ya kimaksudi ambapo riwaya alizozifanyia utafiti aliziteua kwa kudhamiria kuwa zilisheheni maudhui mengi yaliyohusu changamoto halisi zilizowakabili vijana katika jamii yao. Data iliyokusanywa ilijumuisha maudhui yenye changamoto halisi zilizowakabili vijana kama vile ufisadi, ubaguzi, umaskini na ukabila. Utafiti huu ulinuiwa kuwa na natija kwa wasomi, wahakiki na watafiti wa masuala ya lugha na fasihi kwa kuwa sehemu ya kurejelewa na pia kuhamasisha   jamii kuhusu changamoto za vijana ili kusaidia kutafuta suluhu kwa changamoto hizo.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here