
Uchanganuzi wa Maudhui na Wahusika Kibibliotherapia katika Hadithi Fupi Teule za Kiswahili
Author(s) -
Rose Mavisi,
Gwachi Mayaka,
Wendo Nabea
Publication year - 2020
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v2i1.128
Subject(s) - physics , humanities , art
Bibliotherapia ni mbinu muhimu inayoweza kutumiwa kama kipumuo kwa vijana kwa baadhi ya matatizo yanayowakumba katika kipindi fulani cha maisha yao. Bibliotherapia humsaidia msomaji kupitia mtagusano wake na maudhui na wahusika ambao wamepitia hali kama ya yule msomaji. Makala haya yalilenga kuchanganua maudhui na uhusika ili kubaini sifa za kibibliotherapia katika diwani hizi za hadithi fupi; Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine (2004), Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine (2007), Kiti cha Moyoni na hadithi nyingine (2007) na Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (2016). Mbinu iliyotumiwa kukusanya data hii ni majadiliano katika makundi au kundi lengani. Utafiti huu ulipata matini yake kutoka kwa hadithi fupi teule zinazotumiwa au zinazoweza kutumiwa kama matini ya fasihi ya Kiswahili katika shule za upili. Utafiti huu ulichukua sampuli kutoka kwa shule 7 za Serikali katika eneo la utafiti. Eneo la utafiti ni kaunti ya Nairobi. Sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu zifuatazo; kimakusudi, kinasibu na utabakishaji. Watafitiwa walikuwa walimu 28 pamoja na wanafunzi 112 wa Kidato cha Tatu wa fasihi ya Kiswahili ambao walizisoma hadithi fupi teule na kutathmini sifa za kibibliotherapia.Kazi hii iliongozwa na mihimili ya nadharia ya Mapatano ya Mwitikio wa Msomaji yake Rosenblatt (1995). Mijadala ya kundi lengani ilionyesha kwamba hadithi fupi zinazosomwa darasani ni za kuaminika na maudhui yanaeleweka vizuri .Ufaafu wa maudhui na wahusika kwa mahitaji ya wanafunzi ni muhimu ili faida za kibibliotherapia zipatikane.