
Uchambuzi wa Maudhui katika Matangazo ya Ngono-Salama kwenye Ukurasa wa Shabiki wa Durex Facebook
Author(s) -
Douglas Nkumbo,
Sheila Wandera-Simwa,
James Onyango Ogola
Publication year - 2019
Publication title -
editon consortium journal of kiswahili
Language(s) - Spanish
Resource type - Journals
ISSN - 2663-9289
DOI - 10.51317/ecjkisw.v1i1.43
Subject(s) - humanities , art
Usomi huu ulinuia kuchanganua matangazo ya ngono salama katika mtandao wa Facebook wa Durex. Utafiti huu ulihusu mada ambazo ni mwiko katika jamii kwa kuangazia matangazo ya ngono salama. Madhumuni ya utafiti ni kubainisha na kuchanganua maudhui ambayo yanasisitizwa katika matangazo ya Durex katika mtandao wa Facebook, kudhihirisha uhalalishaji wa matangazo ya ngono salama ili kuwashawishi wateja wengi kununua na kutumia bidhaa zao. Utafiti huu ulitumia Nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi hasa kwa kuzingatia muundo wa Fairclough wa 3D na muundo wa Kress Van Leuuwan wa Isimu ya picha.Muundo wa utafiti huu ni wa kiuthamano na kimaelezo. Data ilikusanywa kwa kutazama na kusakura matangazo ya Durex katika mtandao wa Durex. Sampuli ya data ilifanywa kimakusudi kisha ilihifadhiwa kieletroniki ili kuafikia malengo ya utafiti huu, ambapo matini za picha mia moja hamsini (150) zilichaguliwa na kuchanganuliwa. Matokeo ya Utafiti huu yanadhirisha kwamba maudhui yanayosisitizwa ni hisi za raha bila kuweka wazi ashiki za ngono, durex wanatumia mbinu ya uhalalishaji wa matangazo yao ili kushawishi wateja. Utafiti huu utawafaa wasomi wa isimujamii hasa katika mawasiliano ya afya. Pia usomii huu utasaidia kuziba pengo la changamoto ya kimawasiliano ya mada ambazo ni mwiko kwa wanaondaa matangazo ya ngono salama katika jamii ili matangazo ya ngono salama yaandiliwe ambayo yanakukubalika na jamii nyingi. Hatimaye matokeo ya utafiti yatasaidia wanaoandaa mitalaa ya elimu ili kuhusisha na kuhamasisha umma kuhusu elimu ya ngono salama kwa kutumia mitandao ya kijamii.