z-logo
open-access-imgOpen Access
UCHUNGUZI WA UUNDAJI WA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KATIKA TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA
Author(s) -
Margaret June Achieng` Mung`ala,
George Obara Nyandoro,
Charles Nyandoro Moochi
Publication year - 2020
Publication title -
american journal of education and practice
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
ISSN - 2520-3991
DOI - 10.47672/ajep.560
Subject(s) - theology , philosophy
Utafiti huu ulichunguza uundaji wa vitambulisho vya utaifa katika tamthilia ya Mstahiki Meya, Arege (2009).Tamthilia ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa mbele ya hadhira au ni kazi iliyoandikwa ili kusomwa na hadhira. Isitoshe maagizo haya huakisi hali halisi katika jamii. Lengo kuu la kutunga tamthilia ni kuadilisha na kuwawezesha wananchi kutambua baadhi ya mambo yanayotendeka katika jamii halisi kwa kuwa, fasihi ni ukweli wa maisha. Vitambulisho ni sifa, hisia ama imani ambazo humtofautisha mtu au kabila au raia wa nchi fulani na nyingine. Huku utaifa ni hali ambapo wananchi wote hujitambua kuwa sawa katika taifa fulani na hushiriki kwa pamoja katika kuleta amani na maendeleo taifani mwao.Utafiti huu ulinuia kujibu swali lifuatalo, Kwanza, dhana ya vitambulisho vya utaifa vimejitokezaje kwa mujibu wa tamthilia ya Mstahiki Meya? Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhistoria mpya ikishirikiana na nadharia ya utaifa. Umuhimu wa utafiti huu ni kwamba, utaongeza maarifa katika nadharia na mbinu za uhakiki wa tamthilia za Kiswahili nchini Kenya, kwa kurejelea na kuweka wazi vitambulisho vya utaifa, pia utaweza kutumika katika taaluma ya fasihi hususan tamthilia, kama marejeleo na itawasaidia wanafunzi na watafiti watakaotaka marejeo ya tamthilia ya Kiswahili nchini Kenya ili kuweka wazi vitambulisho vya utaifa na jinsi vinavyojitokeza  katika tamthilia, vilevile ni malighafi kwani utatoa mchango mkubwa katika historia ya tamthilia nchini Kenya na kutajirisha maktaba ya chuo kikuu cha Kisii. Aidha, tume ya utangamano wa taifa nchini Kenya (NCIC), itagundua umuhimu wa fasihi kupitia tamthilia, katika uundaji wa vitambulisho vya utaifa inayoendeleza utangamano nchini hivyo basi itawawezesha kufadhili tafiti zitakazonuia kushughulikia suala hili. Uchunguzi huu ulifanywa maktabani. Muundo wa utafiti uliotumiwa ni utafiti elezi. Kwa hivyo matokeo yaliwasilishwa kupitia maelezo

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here