
Kiswahili Katika Taathira ya Kihistoria na Mielekeo ya Kisiasa kama Lugha ya Kufundishia
Author(s) -
Gerephace Mwangosi
Publication year - 2018
Publication title -
mkwawa journal of education and development
Language(s) - Bosnian
Resource type - Journals
ISSN - 2453-6059
DOI - 10.37759/mjed.2018.2.1.3
Subject(s) - theology , philosophy
Makala hii inahusu Kiswahili katika taathira ya kihistoria na mielekeo ya kisiasa kama lugha ya kufundishia elimu ya juu hapa nchini Tanzania. Makala hii inaeleza mambo yanayosababisha mielekeo tofauti ya watu kuhusu upokezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia elimu ya juu nchini Tanzania ili kushurutishaukubalifu wake. Baadhi ya masuala yanayochunguzwa ni yale yanayotiliwa shaka kuhusu uwezo wa lugha ya Kiswahili kumudu na kukidhi harakati za mahitaji ya kufundishia elimu ya juu, pamoja na kupitisha teknolojia mpya inayoinukia katika nyanja za sayansi nateknolojia. Aidha, makala hii inanuia kufafanua ukubalifu, pamoja na msingi wa mielekeo ya Watanzania kutoipatiakipaumbele lugha ya Kiswahili kama lugha inayoweza kukidhi mahitaji ya kufundishia elimu ya juu hapa nchini. Data za msingi katika makala hii zilipatikana maktabani kwa kudurusu nyaraka mbalimbali zilizohusiana na mada iliyolengwa. Mapitio ya nyaraka mbalimbali zilizotumika kushadidia data za msingi za mada iliyochunguzwa zilipatikana katika maktaba ya chuo kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha iliyopoIringa. Makala hii inahitimisha kwamba lugha za kigeni na zile za kiasili zinaweza kuendelea kutumika pamoja katika ngazi zote za elimu ili kuziwezesha kutekeleza vema dhima zake.