
Dhamira za Maandishi ya Kuta za Vyooni Jijini Dar es Salaam
Author(s) -
Willy Migodela
Publication year - 2017
Publication title -
mkwawa journal of education and development
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
ISSN - 2453-6059
DOI - 10.37759/mjed.2017.1.1.2
Subject(s) - humanities , art
Makala haya yanahusu dhamira za maandishi, hususani ya vyooni Jijini Dar es Salaam. Lengo ni kuangalia dhamira za maandishi hayo na nafasi yake kwa jamii. Katika uchambuzi tumetathmini ubunifu unaojitokeza katika maandishi hayo. Aidha, kwa kutumia mbinu za utafiti maktabani kama vile uchambuzi matini na mbinu za uwandani, tulipata data muafaka kuhusu suala la kiutafiti lililoshughulikiwa katika makala haya. Pia, tumedurusu maandiko mbalimbali yanayozungumzia dhamira katika maandishi yaliyoandikwa sehemu mbalimbali na namna lugha ilivyotumika kutoa mawasiliano. Aidha, tumetumia nadharia ya Elimu-mitindo ambayo ndiyo inayoongoza uchambuzi na mjadala katika makala haya. Hali kadhalika, kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa dhamira zilizojitokeza zaidi ni zile zinazohusu maradhi, maarifa, maadili na dini. Ilibainika pia kuwa dhamira hizi zinaakisi muundo na mfumo wa maisha ya jamii husika. Kutokana na matokeo haya, imehitimishwa kuwa ubunifu uliopo kwenye maandiko ya vyooni unasawiri hali mbalimbali katika jamii kama vile mtazamo wa wanajamii kuhusu maana na umuhimu wa elimu, dini, maadili na utamaduni kwa ujumla. Hatimaye, katika makala haya tutaona jinsi lugha safihi (matumizi ya lugha yasiyo na adabu) inavyojitokeza katika maandishi ya vyooni.