z-logo
open-access-imgOpen Access
Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi
Author(s) -
Cheruiyot Evans Kiplimo,
Leonard Chacha Mwita
Publication year - 2022
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Spanish
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.5.1.527
Subject(s) - humanities , art
Kiswahili ni lugha mojawapo ya Kiafrika inayochangia ujifunzaji wa fonolojia. Wanaisimu wamejadili mifanyiko ya kifonolojia katika Kiswahili bila kugusia swala la athari zake katika vipashio vikubwa kuliko fonimu. Hata hivyo, siyo mifanyiko yote ya kifonolojia ndio huathiri fonolojia arudhi ya lugha husika. Fonimu zinapoungana ili kuunda vipashio vikubwa vya lugha kama vile silabi na neno, zinaathiriana katika viwango mbalimbali. Athari zingine huwa ndogo kiasi kwamba hazionekani bayana ilhali athari zingine huwa kubwa kiasi cha kuonekana bayana. Mfanyiko wa kifonolojia unaohusishwa na utowekaji wa fonimu ni udondoshaji. Fonimu inapotoweka katika neno, vipashio vikubwa kuliko fonimu yenyewe hupokea athari katika mfumo wa lugha. Makala hii inaonyesha jinsi mabadiliko ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi huathiri fonolojia arudhi ya Kiswahili. Hili liliwezekana kwa kujenga umbo la awali la neno kisha kuonyesha jinsi kudondoshwa kwa fonimu kuliathiri fonolojia arudhi. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya fonolojia zalishi iliyoasisiwa na Chomsky na Halle (1968). Makala hii, imetegemea data ya maktabani iliyokusanywa kwa kusoma, kudondoa na kunakili.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here