z-logo
open-access-imgOpen Access
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Author(s) -
Furaha J Masatu,
Venancia F Hyera,
Osmunda R Ndunguru
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Bosnian
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.4.1.512
Subject(s) - humanities , art
Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili. Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu. Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu. Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto. Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu. Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume. Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008). Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea. Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu. Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume. Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto. Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here