
Utumikizi wa Mwingilianotanzu katika Fasihi ya Watoto
Author(s) -
Caroline Nyambura Muriithi,
Boniface Ngugi
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Uncategorized
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.4.1.439
Subject(s) - ancient history , theology , history , philosophy
Tanzu zimeendelea kujidhihirisha katika umbo la riwaya na kuifanya mseto wa mambo mbalimbali. Kutegemeana na kuathiriana kwa tanzu kunaitwa mwingilianotanzu. Fasihi ya watoto imeendelea kukua na kudhihirisha matumizi ya tanzu mbalimbali katika umbo lake na hivyo kuwa changamano. Uchangamano huu unatatiza upokeaji na uelewekaji wa dhima yake, hasa ikizingatiwa kuwa riwaya hizo zinatumika katika mtaala wa elimu nchini. Makala haya yananuia kufafanua ni vipi mwingilianotanzu unavyojisawiri katika vitabu vya fasihi ya watoto. Mifano itatokana na baadhi ya vitabu teule vya fasihi ya watoto ni Habari za Mawio (Masoud Nassor) na Maskini Bibi Yangu! (Said A Mohamed). Mwishowe itapendekeza namna mwingilianotanzu unavyoweza kutumiwa kwa ufaafu zaidi katika uelekezaji wa usomaji na kuuwasilisha ujumbe katika fasihi ya watoto.