
Taswira ya Mwanamke katika Kipindi cha Bi. Msafwari Runinga ya Citizen Nchini Kenya.
Author(s) -
Janet Jepkurui Kibet,
Rebecca Wanjiru Omollo,
Rose Mavisi
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Spanish
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.3.1.430
Subject(s) - humanities , art
Utafiti huu unalenga kuchunguza na kutathmini taswira ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari Katika runinga ya Citizen nchini Kenya kwa mtazamo wa kifasihi. Utafiti huu uliongozwa na lengo lifuatalo: Kueleza nafasi ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari Katika runinga ya Citizen nchini Kenya. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi mathalani Ufeministi wa Kiafrika na nadharia ya mtindo. Nadharia ya Ufeministi ilifaa utafiti huu kwa kuwa inashughulika na masuala ya kijinsia hasa jinsia ya kike. Muundo wa kimfano ulitumika katika uchanganuzi wa utafiti huu. Utafiti huu ulijikita katika maktabani ili kupata maandishi yanayohusiana na mada iliyoshughulikiwa. Kutokana na maelezo haya, kundi lengwa la utafiti ni kipindi cha Bi. Msafwari Katika runinga ya Citizen. Sampuli iliyotumika ni sampuli ya kimaksudi ambayo kipindi cha Bi. Msafwari kiliteuliwa. Utafiti huu ulitumia mbinu ya kutazama, kusikiliza na kurekodi vipindi katika kukusanya data yake. Matokeo ya utafiti yalijitokeza wazi kuwa, nafasi ya mwanamke ni: kumfurahisha mume wake, kumsaidia mume wake, kutii, kumheshimu na kunyenyekea mbele ya mume. Pia ana nafasi ya kudumisha amani katika ndoa. Ukusanyaji na uchanganuzi wa data, uwasilishaji wa matokeo ulifanywa kwa njia ya maelezo. Utafiti uliofanywa utawafaa watafiti wengine watakaojishughulisha na mada inayohusu mwanamke kwani wataweza kurejelea kazi hii ili kupata habari kuhusu nafasi ya mwanamke. Kwa ujumla, utafiti uliyofanywa ulichunguza taswira ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari.