z-logo
open-access-imgOpen Access
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Author(s) -
Grace Adhiambo Onyango,
Onesmus Gitonga Ntiba,
Rocha Chimerah
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.3.1.413
Subject(s) - humanities , philosophy
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe na kukiuka uhalisia. Riwaya ya Babu Alipofufuka ya Mohamed ni mfano mojawapo wa fasihi yenye uhalisia-mazingaombwe. Utafiti huu unapambanua mkabala huo kwa kusimikwa kwenye mada Mustakabali wa Uongozi katika bara la Afrika katika karne ya 21: Tathmini ya Uhalisia-ajabu katika Riwaya ya Babu Alipofufuka na Said Ahmed Mohamed. Malengo ya utafiti huu ni; Kupambanua uhalisia-ajabu na uozo wa uongozi na hatimaye kutambua suluhu kwa matatizo ya uongozi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya ya Babu Alipofufuka. Uchunguzi katika kazi hii uliongozwa na nadharia ya uhalisia-ajabu kwa kujifunga kwa mihimili yake mitano: kinaya, uandishi ndani ya uandishi, umazingaombwe katika mukhtadha halisi, vurugu la kiwakati na muingilano wa matini. Utafiti wenyewe uliendeshwa kwa mtindo wa kimakusudi ambapo matini maalum zilichanganuliwa maktabani na vile vile mtandaoni. Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Mhakiki pia alilenga kuchanganua kazi nyingine za fasihi kwa misingi ya malengo ya utafiti huu. Matokeo ya uchunguzi huu yana umuhimu mkubwa kwani yatasaidia kuchunguza suala la uongozi katika kutatua matatizo ya ndani kwa ndani kwa mustakabali wa itikadi za Kiafrika. Uchunguzi huu unashikilia kuwa utandawazi ni nduli ambalo limechangia kuwepo kwa matatizo humu barani na kuzidi kuifanya Afrika kunyongeka katika minyororo ya utumwa mpya. Taswira hii ni dhahiri katika riwaya mpya za Kiswahili. Matokeo yake bila shaka yatapevua ufahamu kuwa Afrika ina itikadi za kijadi ambazo zilizingatiwa katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya ndani kwa ndani hasa za kisiasa. Wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu pia watanufaika na matokeo ya uchunguzi huu kwa kupata mwelekeo wa uhakiki wa kazi za fasihi mintarafu zenye uhalisia-ajabu.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here