
Jinsi Watoto Wanavyokabiliana na changamoto kwenye vitabu vya fasihi
Author(s) -
Viola Jepkemboi Kiplagat,
Rebecca Wanjiku Omolo,
Margan Adero
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Bosnian
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.3.1.405
Subject(s) - physics
Watoto wengi wanapitia changamoto nyingi miongoni mwa walezi wao na wanajamii. Kutokana na yale wanayoyapitia pamoja na mazingira duni wanamoishi, watoto wengi hukosa mwelekeo dhabiti wa kimaadili hivyo basi kukosa mahitaji yao ya kuwawezesha kuwa na hulka zinazokubalika katika jamii. Mtafiti alinuia kuchanganua vitabu vya fasihi ya watoto ili kubainisha iwapo vitabu hivi vinaweza kutekeleza mahitaji ya watoto kupitia migogoro au changamoto vitabuni. Vitabu teule vilivyotumiwa katika utafiti vilikuwa Ahaa! Roda (2017) kilichoandikwa na Tom Nyambeka na Mwisho wa Ujambazi (2017) naye Yahya Mutuku. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Maadili na nadharia ya Uhalisia. Njia za utafiti zilizotumiwa ni hojaji na upekuzi wa yaliyomo kwenye vitabu teule vya fasihi ya watoto. Data iliyokusanywa ilipangwa kulingana na maswali ya utafiti na kuchanganuliwa kwa kuzingatia mkabala mseto ambapo, muundo wa QUAL-QUAN ulitumika. Mtafiti alichanganua vitabu teule vya fasihi kimaelezo akiongozwa na maswali ya utafiti. Mtafiti alikusanya data nyanjani kupitia hojaji zilizosambazwa kwa sampuli ya asilimia kumi ya watoto mia mbili kutoka darasa la saba, shule ya msingi ya Langas, Kaunti ya Uasin Gishu. Shule hii ya Langas ni shule iliyoko katika mazingira duni hivyo basi watoto wengi wanapitia changamoto nyingi za kijamii. Matokeo yalibainisha kuwa vitabu vya fasihi vinaweza kutekeleza mahitaji ya watoto kupitia migogoro vitabuni na kwamba vitabu vya fasihi ya watoto vinaweza kutoa mwelekeo kwa watoto kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto katika hali halisi. Watoto 50% waliotafitiwa walikubali kuwa vitabu walivyovisoma vilikuwa changamoto ambazo waliweza kufananisha na hali halisi. Changamoto kwenye vitabu teule zilioana na changamoto halisi za watoto. Utafiti huu ulitoa mapendekezo kwa taasisi ya KICD na wizara ya elimu watumie utafiti huu kufanya tafiti zaidi ili kuchangia zaidi mitaala kwa lengo la kutekeleza mahitaji ya watoto. Walezi, walimu, wakuu wa shule watumie utafiti huu kuwalea watoto wao kwa njia mbadala na wenye manufaa. Utafiti zaidi uweze kufanywa kuhusu fasihi ya watoto kutekeleza mahitaji ya watoto kupitia changamoto zinazotokana na migogoro vitabuni. Waandishi wa vitabu pia watumie utafiti huu kuandika vitabu vilivyo na maudhui tofauti tofauti yanayoguza changamoto za watoto na hali halisi ya watoto