
Urudiaji wa Kisarufi Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi
Author(s) -
Aloo Ronald Odhiambo,
Kineene wa Mutiso,
Kyallo Wadi Wamitila
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Uncategorized
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.3.1.404
Subject(s) - humanities , art , theology , history , philosophy
Katika makala haya, tumechunguza aina na mchango wa urudiaji wa kisarufi katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Ili kufanikisha hili, tumeongozwa na nadharia ya Umtindo ambayo inachunguza na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi. Hii ni kwa sababu uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hauwezi kujisimamia. Nadharia ya Umtindo inahusishwa na Geoffrey Leech katika mwaka wa 1969 kutokana na kazi yake ya kwanza ya ushairi alioandika huku akizingatia mawazo ya nadharia hii. Lengo la uhakiki wetu ni kuweka wazi aina mbalimbali za urudiaji wa kisarufi zilizotumiwa katika utenzi huu na michango yake katika kufanikisha fani na maudhui kwenye utungo huu. Baada ya uhakiki wetu, tumegundua kuwa urudiaji wa kisarufi unachangia maudhui, wahusika, vipengele vya kimtindo na vipengele vingine vya fani kwa ujumla katika utungo huu. Isitoshe, urudiaji huu wa kisarufi umekuwa na umuhimu katika kuleta mwangwi na usisitizaji. Tumetumia maelezo na ufafanuzi kutoka katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi kama njia ya kubainisha haya.