z-logo
open-access-imgOpen Access
Nafasi ya Tashbihi katika Kufanikisha Maudhui katika Fasihi ya Watoto
Author(s) -
Ibrahim Matin,
Simiyu Kisurulia
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Bosnian
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/jammk.3.1.355
Subject(s) - humanities , art
Makala haya yalichunguza jinsi wasanii wa vitabu vya fasihi ya watoto wamefuma tashbihi katika kazi zao ili kueleza maudhui yanayowalenga watoto kwa kuongozwa na nadharia ya umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916). Kupitia kwa njia ya kiupekuzi na uchanganuzi matini, vitabu vya Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwana viliteuliwa kimakusudi, vikasomwa na kuchanganuliwa. Tashbihi mbalimbali na maudhui ya familia, elimu, nidhamu, bidii, ugonjwa na kifo yalitambuliwa na kujadiliwa kwa undani. Uhusiano kati ya tashbihi na maudhui hayo ulidhihirishwa. Matokeo ya jinsi tashbihi zinavyofanikisha kueleza maudhui yaliwasilishwa kithamano. Utafiti huu umeonyesha tashbihi na maudhui katika kazi tulizohakiki na pia unachochea washikadau katika uwanda wa fasihi ya watoto kuhakiki kazi za watoto kabla kuwateulia kuzisoma.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here