
Tathmini Linganishi kati ya Mtalaa wa 8.4.4 na wa Umilisi wa 2.6.6.3 katika Ufundishaji wa Fonimu za Kiswahili katika Kiwango cha Chekechea
Author(s) -
Nabangi Joan Wataka,
Susan Chebet Choge,
Luganda Musavi Manasseh
Publication year - 2021
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Polish
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.3.1.267
Subject(s) - humanities , art
Mtalaa ni mpangilio ambao huweka malengo katika ufunzaji wa wanafunzi. Unatumika kama mwongozo kwa walimu ambao huweka viwango vya matokeo ya mwanafunzi sawia na uwajibikaji wa mwalimu. Nchi ya Kenya imeshuhudia mabadiliko ya mitalaa mbalimbali tangu ilipojinyakulia uhuru. Nafasi ya mtalaa wa uhuru wa 7.4.2.3 ilichukuliwa na 8.4.4 mwaka wa 1985 ambao nafasi yake kwa sasa inachukuliwa na mtalaa mpya wa umilisi wa 2.6.6.3 ambao ulianzishwa mwaka wa 2017. Mitalaa hii imefafanua vipengele mbalimbali kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji na ufunzaji. Kwa hivyo, lengo la nakala hii ni kutathmini kiulinganishi ufundishaji wa fonimu za Kiswahili katika kiwango cha chekechea katika mtalaa wa 8.4.4 unaoondolewa, na katika mtalaa mpya wa umilisi wa 2.6.6.3. Mtalaa wa 7.4.2.3 na wa 8.4.4 iliegemea sana uwezo wa mwalimu, yeye ndiye aliyechukua jukumu kubwa katika mchakato wa ufundishaji kuliko wanafunzi. Tofauti na mitalaa hiyo miwili, mtalaa wa 2.6.6.3 unampa mwanafunzi jukumu kubwa katika mchakato wa ujifunzaji kuliko mwalimu. Makala haya pia yamechunguza kiulinganishi ubora na udhaifu wa mbinu mbalimbali za ufundishaji wa fonimu za Kiswahili katika kiwango cha chekechea katika mitalaa ya 8.4.4 na mpya wa 2.6.6.3. Nadharia ya Piaget ya Utambuzi imeongoza makala haya. Makala haya yanaripoti baadhi ya matokeo ya utafiti uliofanywa kwa minajili ya shahada ya uzamili katika Elimu ya Kiswahili.