z-logo
open-access-imgOpen Access
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Author(s) -
Peter T Mramba
Publication year - 2020
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Polish
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.2.2.242
Subject(s) - art
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo. Aidha, malengo mahususi: kubainisha silabi inayohusishwa na Tonijuu Msingi (kuanzia sasa TJM) na mbili, kujadili ruwaza ya utokeaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala hutokeaji huo. Data ya Makala haya imetokana na utafiti mpana uliofanywa juu ya toni katika wilaya ya Rombo (2019) ambao   uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya fonolojia. Aidha, mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni pamoja na mahojiano na ushuhudiaji. Katika mahojiano vitenzi visoukomo changamani viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuvitamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika vitenzi hivyo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwapo au kutowapo kwa yambwa. Aidha, vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa toni chini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi visoukomo changamani vya silabi mbili hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya udondoshaji wa TJM pamoja na kanuni nyingine kitoni kama vile: kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja. Aidha, TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina. Pia, matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi.  Makala haya yamesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo kwa ujumla.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here