z-logo
open-access-imgOpen Access
Nafasi ya Fasihi Katika Kuwasilisha Masuala ya Mazingira Kupitia Riwaya Teule Tikitimaji (2013) na Msimu wa Vipepeo (2006) za K. W. Wamitila
Author(s) -
Esther Lucy Wesonga,
Beverlyne Asiko Ambuyo,
Rocha Chimerah
Publication year - 2020
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.2.2.192
Subject(s) - art , humanities
Suala la mabadiliko ya hali ya anga ni janga linaloendelea kukumba ulimwengu kwa jumla. Kutokuwepo kwa usawazishaji wa ekolojia ni jambo ambalo linawatia shaka adinasi wengi. Fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kuwasilisha hali halisi ya maisha ya binadamu. Utafiti huu unachambua nafasi ya fasihi katika kuwasilisha masuala ya mazingira kupitia riwaya mbili teule za Wamitila, Tikitimaji (2013) na Msimu Wa Vipepeo (2006). Mwandishi huyu ameonyesha ari katika uwanja wa fasihi mazingira, kwenye makala yake ya “Place and placelessness in Kiswahili literature: The role of setting in Kiswahili creative writing” anasema kuwa mandhari huchukua nafasi katika kuwasilisha masuala ya mazingira. Kazi hii ilichunguza namna mwandishi alivyotumia fasihi kuwasilisha masuala ya mazingira katika riwaya zake za hivi karibuni. Ingawa kwa miaka mingi, masuala ya mazingira yamehusishwa na sayansi haswa katika kutoa takwimu kamilifu kuhusiana na masuala ya mazingira, fasihi inaendelea kuchukua dhima mpya katika jamii inayozidi kukua kiteknolojia. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni yafuatayo: kubainisha jinsi mwandishi wa riwaya ya Tikitimaji alivyotumia wahusika ili kuwasilisha maudhui ya mazingira. kueleza mitindo ya lugha iliyotumiwa kuwasilisha masuala ya mazingira na tatu, kutathimini iwapo mwandishi amefaulu kuwasilisha maudhui ya mazingira riwayani. Utafiti huu ulitumia kiunzi cha nadharia kutoka kwa nadharia ya fasihi mazingira na nadharia ya uhalisia. Mihimili zitakazotumiwa kutoka nadharia ya uhalisia ni: kazi ya fasihi imejitosheleza, kazi ya msanii inapaswa kuwasilisha ukweli, mtunzi anaangalia matatizo na kuchunguza chanzo chake na mwisho wahusika ni vielelezo yakini vya binadamu wa kawaida kwa vile wao hutumia lugha ya kawaida wanayoitumia humwezesha mwanadamu kujifafanulia uwezo wake wa kutenda mambo. Mihimili ya fasihi mazingira iliyotumika ni: kuangalia dhana za ekolojia katika kazi za fasihi, mitindo na uwezo wa lugha na jinsi mitindo hiyo huathiri namna binadamu anavyotagusana na mazingira  na mwisho binadamu hawezi ishi bila ekolojia lakini ekolojia huweza kuishi bila binadamu. Data ilipangwa kwenye makundi na kuchanganuliwa kwa kuzingatia madhumuni ya utafiti na mihimili ya kiunzi cha nadharia. Data iliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umelenga kuhamasisha wasomi na waandishi wa fasihi wajikite zaidi kulenga masuala ya mazingira ambayo ndicho kitovu cha maisha ya binadamu. Utafiti ulibaini kuwa fasihi ni nyenzo mwafaka ya kuwasilisha masuala ya mazingira kupitia vipengele vyake. Kwani huingiliana sana na utamaduni wa jamii.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here