z-logo
open-access-imgOpen Access
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Author(s) -
Fred Wanjala Simiyu,
Margan Adero,
Joyce Chepkwony
Publication year - 2020
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Uncategorized
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.2.2.183
Subject(s) - humanities , physics , art
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo. Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo. Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka. Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa.  Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972. Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga. Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini. Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School. Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70. Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa. Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here