z-logo
open-access-imgOpen Access
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Author(s) -
Willy Wanyenya
Publication year - 2020
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Spanish
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.2.2.169
Subject(s) - humanities , art
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Kwa kurejelea jamii hii, mtafiti anaeleza namna wazazi wanavyotumia lugha kuelekeza mabinti zao katika mambo yanayopelekea ndoa zao kudumu.  Mtafiti alinukuu baadhi ya semi ambazo zinasemekana kuwa zinatumiwa na wazazi katika shughuli hiyo. Ni kweli kwamba lugha yoyote ile huwa inafanya kazi nyingi sana kama vile kutumbuiza watu, kutongozana, kugombana, kufundisha, kuelekeza, n.k. Hii ni kwa sababu bila kutumia lugha, mtu hawezi akaimba wimbo, akagombana, akafundisha, na akaelekeza. Hata hivyo, katika makala hii, mtafiti anajikita kwenye mchango wa lugha katika maisha ya ndoa. Katika kazi hii, mtafiti anazingatia semi mbalimbali ambazo Wamasaaba huzitumia kwa ajili ya kuelekeza mabinti zao katika masuala ya ndoa. Katika jamii mbalimbali, watu hutumia lugha kutekeleza jambo hili. Jamii hasa zile za jadi zilitumia lugha kuelekeza mabinti katika mambo ya ndoa. Kuna namna ambavyo walisuka lugha kisanaa kwa lengo la kufunza mabinti maisha ya ndoa. Hii ni kwa sababu hawakuwa na madarasa maalumu mwa kufunzia watoto wao kama ilivyo sasa. Katika jamii hizo, shule zenyewe hazikuwepo. Kwa hiyo, lugha ndiyo ilikuwa chombo maalumu cha kufunzia watoto. Matumizi ya lugha yalidhamiria kukuza mabinti ambao wangevumilia maisha ya ndoa. Hivyo basi, katika kazi hii, mtafiti anajikita katika matumizi ya lugha na kueleza jinsi Wamasaaba wanavyotumia semi mbalimbali kuelekeza mabinti zao katika masuala ya ndoa.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here
Accelerating Research

Address

John Eccles House
Robert Robinson Avenue,
Oxford Science Park, Oxford
OX4 4GP, United Kingdom