z-logo
open-access-imgOpen Access
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Author(s) -
Willy Wanyenya
Publication year - 2020
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Slovenian
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.2.2.159
Subject(s) - tanzania , humanities , art , history , ethnology
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo kwa kila mwanafunzi unapofika, wanafunzi huwa na sababu za kimsingi zinazowafanya wapendelee masomo fulani na kuyakataa mengine. Kwa kawaida wanafunzi huwa hawalazimishwi kuchukua masomo fulani. Kila mwanafunzi huwa na uhuru wa kuchagua masomo anayoyapenda. Imebainika wazi kuwa nchini Uganda, wakati wa wanafunzi kupunguza idadi ya masomo unapofika, wengi wao huwa wanaacha somo la Kiswahili. Katika darasa la wanafunzi mia moja, ni wanafunzi kumi au kumi na watano tu ndio wanachukua Kiswahili. Hali hii inatisha sana hasa kwa wapenzi wa Kiswahili. Hivyo basi, mtafiti aliendeleza utafiti huu ili kueleza sababu zinazopelekea wanafunzi kufanya hivyo. Dhamira ya utafiti ni kueleza bayana kwa nini wanafunzi wengi nchini Uganda huwa hawachukui somo la Kiswahili. Madhumuni ya utafiti huu ni kueleza mielekeo ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda dhidi ya ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili na kufafanua hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa ili kufanya idadi ya wanafunzi wa Kiswahili iongezeke. Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Utafiti huu umeonyesha kuwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda huwa hawapendelei somo la Kiswahili kwa sababu zifuatazo: kuwepo na sera mbovu nchini kuhusu lugha ya Kiswahili; wanafunzi kutokuwa na msingi wa lugha ya Kiswahili; wanafunzi kuwa na fikra potovu kuwa Kiswahili ni lugha ya wezi; wanafunzi kufikiria kuwa Kiswahili ni somo linalofaa wenzao kutoka Kenya na Tanzania; wanafunzi kufikiria kuwa lugha ya Kiswahili ni ngumu; watu wa nchi ya Uganda kuchukulia Kiswahili kuwa lugha ya kawaida na isiyofaa kufundishwa shuleni; wananchi wa Uganda kupendelea Kiganda na Kiingereza na kupiga vita lugha ya Kiswahili.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here