z-logo
open-access-imgOpen Access
‘Siyasa ni Tʰanga si Nanga’ Mwangwi wa Funzo la Kisiyasa na Azimiyo la Abd̪ilat̪if Abd̪alla Kifungoni: Ut̪afit̪i Kiyelelezo wa Kutendana Katika Sauti ya Dhiki
Author(s) -
Mohameḍ Karama,
Issa Mwamzandi,
Khalid Kitito
Publication year - 2020
Publication title -
east african journal of swahili studies
Language(s) - Spanish
Resource type - Journals
eISSN - 2707-3475
pISSN - 2707-3467
DOI - 10.37284/eajss.2.1.144
Subject(s) - humanities , art
Shairi la Kutendana katika Sauti ya Dhiki limechanganuliwa, mpaka sasa, kwa maono ya juujuu kwamba ni shairi la kingono. Kut̪okana na hit̪imisho hili, Mulokozi amelipuuza kuwa ni shairi lililokosa ubingwa wa kuenreleza maudhui muhimu yanayotatiza jamii. Makala haya yamebayanisha shairi hili kuwa ni fumbo la kisiyasa. Kwa kutumiya madhumuni ya ulingamanishaji wa fasiri ya matukiyo halisi ya kisiyasa katika Kenya wakat̪i huwo na shairi lenyewe; azimiyo la Abd̪ilat̪if katika shairi lenyewe na namna lilivofikiwa; na namna azimiyo hilo lilivoathiri msimamo wake wa kisiyasa baad̪a ya kut̪oka kifungoni, tumeweza kuibuwa maswala muhimu kuhusu maisha ya Abd̪ilat̪if kabla, wakat̪i wa, na baad̪a ya kut̪oka kifungoni. Nadhariya ya Usemezano yenye kud̪ulisha maana kut̪okana na usuli, athari, na mwingiliyano wa kauli nyingi katika mat̪ini na Uhistoriya Mpya yenye kut̪owa fasiri ya matukiyo ya kihistoriya nrizo nadhariya zilizotumika katika uchanganuzi wetu. Kauli mbalimbali zilizojit̪okeza katika mashairi kadhaa ya Sauti ya Dhiki na jazanra zilizotumika zimeweza kufumbuwa ist̪iyara ya shairi hili la Kutendana. Tumeona wahusika wake (wanawake wawili) wanawakilisha vyama va kisiyasa va wakat̪i huwo: KANU (KADU), KPU, na Mwanamume anawakilisha wananchi wa Kenya. Tukiengezeya, Abd̪ilat̪if anajisaili huko gerezani na kupelekeya afanye azimiyo la kujit̪owa katika siyasa za kijumuiya sizisothabit̪i na kuwanasihi wasomaji wengine wasiingiye katika mtego aliyouwingiya yeye. Maisha yake ya kisiyasa baad̪a ya kifungo yanaonekana kufuwata funzo na azimiyo hili.

The content you want is available to Zendy users.

Already have an account? Click here to sign in.
Having issues? You can contact us here